Ijumaa 5 Septemba 2025 - 18:28
Kiongozi wa Jamaat-e-Islami Pakistan: Kujitolea kwa Iran katika kuiunga mkono Palestina ni fahari kwa Umma wa Kiislamu

Hawza/ Hafiz Naeemur Rehman katika hotuba yake alisisitiza kwamba kujitolea kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kuliunga mkono taifa la Palestina ni chanzo cha fahari kwa umma wa Kiislamu na kielelezo cha thamani kwa nchi nyingine za Kiislamu.

Kwa mujibu wa taarifa ya idara ya tarjama ya  Shirika la Habari la Hawza, Hafiz Naeemur Rehman, kiongozi wa Jamaat-e-Islami Pakistan, katika mkutano wa habari mjini Karachi, pamoja na kutoa ripoti ya safari yake ya hivi karibuni nchini Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, alisisitiza juu ya umuhimu wa kuimarisha uhusiano wa kirafiki na ushirikiano wa pande zote kati ya nchi jirani mbili, Iran na Pakistan.

Akifafanua kuhusu safari hiyo iliyodumu kwa siku nne, alisema: “Wakati tulipo kuwepo mjini Tehran, tulifanya vikao muhimu na viongozi wa ngazi za juu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, wakiwemo Dkt. Masoud Pezeshkian, Rais wa Iran, na Dkt. Seyyed Abbas Araghchi, Waziri wa Mambo ya Nje.”

Kiongozi wa Jamaat-e-Islami Pakistan huku akilisifu jukumu kuu la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kuliunga mkono taifa la Palestina na kupinga njama za utawala wa Kizayuni, alibainisha: “Iran kwa ujasiri na uthabiti imesimama dhidi ya uhusiano na utawala wa Kizayuni, msimo huu thabiti ni mfano wa thamani kwa ulimwengu wa Kiislamu, na sisi pia tunatarajia serikali na taifa la Pakistan kusimama pamoja na Wapalestina kwenye mhimili huo huo wa mapambano.”

Akiashiria kujitolea kwa Iran katika njia ya kutetea malengo ya Palestina, aliongeza: “Kujitolea huku si kwa ajili ya watu wa Palestina pekee, bali ni fahari kwa umma mzima wa Kiislamu, kwa mtazamo wetu, huu ndio mkondo ambao nchi nyingine za Kiislamu, hususan Pakistan, zinapaswa kuufuata.”

Hafiz Naeemur Rehman pia alisisitiza juu ya haja ya kuendeleza ushirikiano wa karibu zaidi kati ya Iran na Pakistan na akasema: “Ushirikiano na uratibu kati ya Tehran na Islamabad unaweza kufanikisha jitihada za kuwasaidia watu wanyonge wa Ghaza na kumaliza uhalifu wa utawala wa Kizayuni.”

Mwisho, alibainisha kuwa: “Kuimarishwa uhusiano kati ya Iran na Pakistan si kwa manufaa ya mataifa haya mawili ya Kiislamu pekee, bali pia kunaweza kuwa msingi wa kuundwa muungano mmoja imara dhidi ya mipango na njama za Uzayuni wa kimataifa.”

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha